Numbers 8:6-11

6 a“Watwae Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli wengine na uwatakase kwa kawaida ya ibada. 7 bIli kuwatakasa fanya hivi: Nyunyizia maji ya utakaso juu yao; kisha uwaambie wanyoe nywele kwenye mwili mzima, wafue nguo zao na hivyo wajitakase wenyewe. 8 cWaambie wamchukue fahali mchanga pamoja na sadaka yake ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta; kisha utamchukua fahali mchanga wa pili kwa ajili ya sadaka ya dhambi. 9 dWalete Walawi mbele ya Hema la Kukutania na ukusanye jumuiya yote ya Waisraeli. 10 eUtawaleta Walawi mbele za Bwana, na Waisraeli wataweka mikono yao juu ya Walawi. 11 fHaruni atawaweka Walawi mbele za Bwana kama sadaka ya kuinua kutoka kwa Waisraeli, ili kwamba wawe tayari kuifanya kazi ya Bwana.

Copyright information for SwhKC